Advertisements
RSS

NBC KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

07 Sep
NBC KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

nbc houseBENKI ya NBC imezindua mpango wa zawadi kwa wateja utakaowawezesha kupata punguzo na ofa kutoka kwa washirika wenye maduka zaidi ya 25 nchini.

NBC wamezindua mpango huo kuwashukuru wao wenye kipato cha juu na cha kati.

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Amana cha benki hiyo, Andrew Massawe amesema, mpango huo ni maalumu kwa wateja wenye akaunti binafsi.

Massawe amesema, washirika wa benki hiyo wanaoweza kupata punguzo la hadi asilimia 30 ya bei halisi ni pamoja na wamiliki wa maduka, migahawa na hoteli.

Kwa mujibu wa Massawe, watakaopenda kufurahia huduma hiyo wanaweza kujiunga na mpango huo baada ya kukidhi vigezo.

“Mteja atapewa kadi maalumu kutoka benki inayomtambulisha kama mwanachama wa Mpango wa kuzawadiwa wateja wa NBC,” alisema.

Alisema katika awamu ya kwanza, huduma zitapatikana kwenye matawi yote ya NBC Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Edward Marks amesema, NBC itaendelea kuwekeza na kuimarisha mtandao wa matawi yake nchini ili kila mteja afurahie huduma za benki hiyo.

Alisema waliamua kuwekeza zaidi kwa kuweka kitengo kinachohusika na wateja maalumu katika tawi la Sea Cliff, Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na kuongeza kitengo kama hicho kwenye tawi la Corporate la jijini humo.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on September 7, 2015 in Business News

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: