Advertisements
RSS

Mkapa: Mkataba wa EPA ni bomu lenye sumu‏

01 Aug

Dar es Salaam

RAIS mstaafu Benjamin Mkapa ameuponda Mkataba wa Pamoja wa Kiuchumi kati ya nchi za Ulaya na Afrika (EPA) kuwa ni bomu lenye sumu na ni mkakati wa mwingine wa nchi tajiri kutaka kupora mali za Bara la Afrika, ikiwamo Tanzania.

Mkapa ameyasema hayo leo wakati anatoa mada kuhusu EPA na athari zake kwa Tanzania katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) jijini Dar es Salaam, Mkapa aliyeufananisha mkataba huo na kikombe chenye sumu, alisema Tanzania iukatae mkataba huo kwani haina cha kupoteza hata kama itakataa kusaini mkataba huo.

Katika mada yake, Mkapa alisema EPA ni mpango wa pili wa kuipora Afrika na akasema mpango huo ni kama ule wa mwaka 1884 na 1885 uliofanyika huko mjini Berlin nchin Ujerumani ambako mataifa 13 yenye nguvu Ulaya yalijadiliana namna ya kugawana na kupora mali za Bara la Afrika.

“Safari hii wamekuja na mfumo huo kupitia EPA iliyozaliwa huko Brussels. Malengo ya Berlin na yale ya Brussels yanafanana kwani yote ni kwa ajili ya kuendeleza biashara na viwanda vya Ulaya,”alisema Mkapa. Brussels ambao ni mji mkuu wa Ubelgiji, ndio makao makuu ya Umoja wa Ulaya (EU).

Mkapa alisema tofauti iliyopo ni kwamba kwa sasa watu ambao wako huru ndio wanatakiwa kusaini makubaliano hayo ya EPA chini ya kivuli cha demokrasia. “Epa ni kikombe chenye sumu ni lazima tuikatae, Waafrika na rafiki wa Afrika lazima waseme sasa,” alisema.

Alisema baada ya mkataba huo wa Cotonou kumalizika muda wake, EU iliingia EPA nyingine na Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2007 na tangu wakati huo hadi sasa, majadiliano ya kuingia kwenye EPA mpya yamekuwa yanaendelea na yameshindwa kupata muafaka kutokana na kuwapo kwa mambo ambayo pande mbili hizo hazikubaliani.

Alisema EU inataka chini ya EPA mpya, nchi za EAC ziingize bidhaa zake barani Ulaya bila kutozwa ushuru na vivyo hivyo nchi za Ulaya zinataka kuingiza bidhaa zake Afrika Mashariki bila kutozwa ushuru. Alisema Umoja wa Ulaya unashikiza mkataba huo mpya utiwe saini haraka kabla ya Januari 2014.

Alisema Tanzania inakabiliwa na uchaguzi wa kusaini au kutosaini mkataba huo mpya ambao kwa sasa unashinikizwa na nchi za Ulaya. Alisema iwapo nchi za Afrika Mashariki zitasaini mkataba huo ni wazi kuwa zitakuwa zimeruhusu asilimia 82.6 ya bidhaa zinazotoka Ulaya ziingie kwao bila kutozwa ushuru.

Alisema kwa Tanzania peke yake takwimu zitaongezeka na kufikia asilimia 90 ya bidhaa kutoka Ulaya zitaingia nchini bila kutozwa ushuru.

“Ni asilimia 10 tu ya bidhaa kutoka Ulaya ambazo zitaingizwa nchini ndizo zitakazotozwa ushuru,” alisema Mkapa na kuongeza kuwa kati ya asilimia hiyo 90, kwa sasa tayari asilimia 23 ya bidhaa zinazotoka Ulaya hazitozwi ushuru na iwapo Tanzania itasaini EPA mpya, itakuwa inaruhusu asilimia nyingine 67 ya bidhaa kutoka barani humo iondolewe ushuru.

Pamoja na ukweli ulio wazi kutokana na maelezo ya raisi Mkapa, Nchi za kiafrika zimekuwa tegemezi kwa nchi zilizoendelea. Je zitaweza kufanya maamuzi yaliyo huru katika mkataba huo? au sababu ya kutegemea misaada kutoka jumuiya ya nchi za ulaya tutalazimika kuingia katika mikataba hiyo mibovu kama wa EPA.

Changia  mawazo yako kwa kutoa  Comment hapo chini. Unadhani Tutaweza kuepukana na hayo?

MJ

Advertisements
 
1 Comment

Posted by on August 1, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , ,

One response to “Mkapa: Mkataba wa EPA ni bomu lenye sumu‏

  1. Richard C Maiko

    August 2, 2012 at 10:14 am

    Tunaweza kwa namna zote kuepuka kusaini mkataba huo wa EPA. ikumbukwe kwamba ni EPA hiyo hiyo ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa nchi kipindi kifupi tu kilichopita kwa kile kilichoitwa account ya madeni ya EPA. Endapo Tanzania ikijiunga na EPA ina maanisha viwanda vyote vya ndani ya nchi vitakufa ; Fuatilia maelezo yafuatayo
    Kiukweli ni kwamba mali ghafi nyingi tunazo tumia kufanya uzalishaji wa kutumia mbinu za kisasa yaani teknolojia zinatoka huko huko Ulaya na tunazipata kwa bei ya juu, gharama za uzalishaji(production costs) nchini Tanzania ni ghali sana kwa sababu ya uhaba wa nishati ambako hupelekea nishati hiyo kuwa ghali sana, hata wataalamu bado tunatoa Ulaya ambao pia ni ghali, hivyo basi bidhaa za kitanzania nighali ukilinganisha na zile za Ulaya, kitu pekee cha kuweza kuzifanya bidhaa za Ulaya zionekane ghali ni ushuru wa kuingiza bidhaa hizo. Kwa hiyo ukiondoa ushuru huo bidhaa hizo zitaonekana zenye bei nafuu kushinda zile za Kitanzania, hivyo basi hakuna atakaye nunua bidhaa za kitanzania zilizo ghali. Swali, tutauza bidhaa wapi kama ndani ya nchi tu vinaonekana ghali? hata hivyo ubora wake nao bado hauridhishi ukilinganisha na zile za Ulaya. Kimsingi ni kwamba hata vitu vya kuuza Ulaya bado hatuna, kwani uzalishaji wetu bado hautoshelezi hata mahitaji ya ndani ya nchi. Yaani kwa kifupi “hatuna comparative advantage wala absolute advantage” katika uzalishaji wa bidhaa yoyote itakayo uzwa ulaya, hivyo basi kusaini mkataba na EPA ni kama tunapoteza muda, na badala ya EPA kuna nchi nyingi za Africa zinazoweza kuwa wateja wa bidhaa zetu kama vile Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na nyinginezo. EPA itatuumiza hakuna cha kufaidika na EPA tuikatae. NGUVU TUNAZO UWEZO TUNAO, TUWE NA NIA TUIKATAE EPA.

     

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: