Advertisements
RSS

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA – SSRA

30 Jul

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA UMMA

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi huu unakwenda sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari na kuleta mkanganyiko miongoni mwa Wanachama na Wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Kufuatia hali hiyo, Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:

 Marekebisho kuhusu kusitisha fao la kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa Mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni.

 Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka Vyama vya Wafanyakazi, Chama cha waajiri pamoja na Serikali.

 Kwa kutambua tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya kazi, tofauti ya sababu za ukomo wa ajira, na umuhimu wa Mwanachama kunufaika na michango yake wakati angali katika ajira, Mamlaka inaendelea na mchakato wa kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya Wanachama. Miongozo na kanuni hizo zitajadiliwa na Wadau wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali kabla ya kuanza kutumika.

 

 Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa Wadau.

 Tangazo hili halitowahusu Wanachama waonachangia katika Mfuko wa Akiba (GEPF), Mifuko ya Hiari (Supplementary Schemes) zinazoendeshwa na PPF,NSSF na LAPF, pia Wanachama waliojitoa kabla ya tarehe 20/07/2012.

 Mamlaka inakanusha vikali kwamba, sitisho la fao la kujitoa si kwa sababu za Kiserikali au kwa sababu Mifuko imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na michango yote ya Wanachama ipo salama.

 Hivyo, Mamlaka inawaomba Wanachama na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya Mwanachama.

 Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji

SSRA-Makao Makuu

 

Advertisements
 
4 Comments

Posted by on July 30, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , ,

4 responses to “TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA – SSRA

 1. Walalahoi

  August 2, 2012 at 8:08 am

  mkakati huu unalenga kudhulumu mafao ya wafanyakazi. itakujaje mtu kupangiwa achukue pesa yake miaka 30 ijayo wakati angekuwa na matumizi nayo leo akiwa na nguvu? Kwanza nani ataidai ikiwa anayekatwa ndiye mwenye uchungu na anajua amelipaje na kwa muda huo serikali inategemea wengi tutakuwa tumekufa? Ina faida gani kwa anayekatwa? Je, Time Value of Money kwa rate anayotaka mhusika atapata? Haiwezekani

  Hii ni duluma na haikubaliki nadhani nayo inafaa mgomo mkubwa maana sasa hili ni janga

   
 2. Bwaksi

  August 29, 2012 at 1:37 pm

  Hawa watu wa SSRA wameleta taharuki kubwa sana, hivi wana ndugu wanachama ktk mifuko ya hifadhi ya jamii, au wanafanya haya kwa shinuikizo la serikali? Maana inaonesha mifuko hii imefilisika na mbinu nzuri ni kulazimisha wanachama tulipwe uzeeni, na huenda kipindi hicho sheria ikawa imebadilishwa tena

   

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: