Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Wabunge wataka Mkurugenzi Bodi ya Pamba atimuliwe‏

23 Jul

Dodoma

WABUNGE wa mikoa inayolimwa pamba, wameitaka Serikali kuhakikisha inamchukulia hatua na kumfukuza kazi Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba kwa madai kuwa ni dikteta, mbinafsi na anachangia kudhoofisha maendeleo ya sekta ya pamba nchini.

Baadhi ya wabunge pia wamelalamikia kiwango kidogo cha bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kilichoombwa pamoja na jumla ya Sh bilioni 52 za bajeti hiyo kwa miradi ya maendeleo kutegemea wafadhili na kuhoji kama dhana ya Kilimo Kwanza inaweza kutekelezwa.

Wabunge hao walikuwa wanachangia hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa mwaka 2012/13 iliyowasilishwa wiki jana na Waziri wa Wizara hiyo, Christopher Chiza, bungeni mjini hapa.

Mbunge wa wa Kahama, James Lembeli (CCM), amesema ,anashangaa kuona bado Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba bado yupo kazini wakati ameshindwa kutekeleza kazi anazowajibika kufanya.

“Mimi nashangaa kwanini mtu huyu anayetusababishia sisi machungu bado yupo, kwa kashfa alizonazo, alipaswa kuwa ameshaondoka, kwa nini Serikali hadi sasa inamlinda, siungi mkono hoja hadi nitakapopata majibu,” amesema Lembeli.

Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), ameilaumu wizara hiyo kuwa imeshindwa kuwakumbuka na kuwasaidia wakulima wa pamba wanaokadiriwa kufikia milioni 16 nchini kutokana na matatizo mengi yanayowakabili.

Alisema wakulima wa pamba wamekuwa wakikandamizwa na wafanyabiashara wa zao hilo, ambao wananunua pamba kwa bei ya chini, akitolea mfano kuwa kilo moja ya pamba imekuwa ikiuzwa Sh 600 wakati uzalishaji wa zao hilo kwa kilo moja kwa mkulima gharama yake ni zaidi ya Sh 800.

“Kama Serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili, tupo tayari kuongozana na wakulima kwenda mahakamani kushitaki wafanyabiashara wote walioingia mkataba na Serikali na kuhamasisha pamba kununuliwa kwa bei ya chini, na kwa hili kwa mara ya kwanza siungi mkono hoja,” alisema Cheyo.

Mbunge wa Busega, Dk Titus Kamani (CCM), alisema matatizo mengi yanayowakabili wakulima wa pamba yanasababishwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba kwa kuwa ni dikteta na mtu hatari anayeweka masharti ili wanunuzi wengi wasiingie kwenye soko la pamba.

Akitoa hoja ya wabunge wanaolima zao hilo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alisema wabunge wote wa maeneo yanayolimwa zao hilo, hawakubaliani na bei ya zao hilo ilivyo chini ya Sh 660 na kuitaka Serikali itafute namna ya kufidia pengo hilo ili wakulima wauze pamba kwa Sh 1,000 kwa kilo.

Akihitimisha hoja hiyo, Waziri  Chiza, alikiri kutambua matatizo ya wakulima wa pamba na changamoto wanazokabiliana nazo kwa kuwa hata yeye ni mmoja wa wakulima wa zao hilo.

Aliwataka wabunge kumpa muda ili aweze kushughulikia changamoto hizo kwa kuwa tangu ateuliwe ni miezi miwili tu imepita.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 23, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: