Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Serikali yatumia mil 361.1/- kutunza kiwanda kilichofungwa‏

23 Jul

Dodoma

SERIKALI imetumia Sh 361,105,009 hadi sasa kwa ajili ya kutunza kiwanda cha Kutengeneza vipuri cha Kilimanjaro (KMTC) na watumishi sita waliobaki tangu kilipofungwa.

Akijibu swali la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) leo bungeni,Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu amesema, serikali hadi sasa imetumia kiasi hicho cha fedha na kwamba Serikali inaendelea kuliweka jengo na mazingira yake katika hali nzuri na ya kuvutia wawekezaji.

Amesema, mwaka 2008, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) lilipokabidhiwa kiwanda walikuwepo watumishi wanane na sasa wapo watumishi sita.

Thamani ya kiwanda kwa sasa ni Sh 11, 491, 133,000. Tathmini inaonesha thamani ya mashine na mitambo ni Sh 3, 279, 133, 000, majengo Sh 5, 162, 000, 000 na ardhi Sh 3,050,000,000.

Amesema, kiwanda kwa sasa ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya viwanda na sekta nyingine za kiuchumi nchini na kuwa Serikali inaendelea kukiweka kiwanda katika hali nzuri, ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati wa majengo ya kiwanda.

Amesema, kwa sasa ukarabati unafanyika kwa awamu na kuwa awamu ya kwanza ya kukarabati majengo ya utawala imekamilika na awamu ya pili itakayohusisha majengo ya karakana yenye mashine na mitambo mingine itafanyika mara fedha zitakapopatikana.

“Mashine na mitambo ya kiwanda hiki ziko katika hali nzuri kwani wafanyakazi wachache waliopo wameendelea kuhakikisha mashine zinafanyiwa uangalizi wa kiufundi wa mara kwa mara,” amesema.

Katika swali lake la msingi, Mbowe alihoji kiwanda hicho ambacho zamani kilikuwa kinazalisha vipuri na kimefungwa muda mrefu, Serikali imetumia kiasi gani cha fedha na watumishi kukitunza tangu kilipofungwa na akataka kufahamu mpango wa Serikali kuzuia uchakavu na upoteaji wa kiwanda hicho na mazingira yake.

Advertisements
 
1 Comment

Posted by on July 23, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , ,

One response to “Kutoka Bungeni: Serikali yatumia mil 361.1/- kutunza kiwanda kilichofungwa‏

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: