Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Serikali kufuatilia upatikanaji sukari‏

21 Jul

Dodoma

SERIKALI imesema kuanzia sasa itafuatilia mwenendo wa upatikanaji wa sukari yote inayozalishwa na inayongzwa nchini mpaka kwa mlaji.
Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Waziri wa Wizara hiyo Christopher Chiza amesema, hadi tarehe 23 mwezi uliopita bei ya rejareja ya sukari katika mikoa yote nchini ilikuwa ni kati ya shilingi 1, 900 na 2,500 kwa kilo.
“Hali hiyo kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na upungufu wa suka katika nchi jirani, kukosekana kwa uaminifu wa wafanyabiashara na mfumo wa udhibiti na usambazaji,” amesema Chiza bungeni leo( Ijumaa) mjini Dodoma.
Waziri Chiza amesema, hadi tarehe 31 Mei, 2012 jumla ya tani 155,972 za sukari ziliingizwa nchini na kwamba hadi tarehe 23 mwezi uliopita tani 29,960 zilikuwa bandarini ambapo pamoja na jitihada hizo bei ya sukari imeendelea kuwa juu.
“Katika mwaka 2012/ 2013 uzalishaji wa suka unatarajiwa kuwa tani 300,906. Kiasi hicho cha sukari pamoja na albaki ya tani 82,911 zilizokwenye maghala ya wafanyabiashara na viwanda kinatarajiwa kukidhi mahitaji ya sukari ambayo ni tani 378,000 kwa mwaka,”alisema.
Amesema, kwa kuwa nchi inazungukwa na nchi zenye upungufu  wa sukari, sukari inayotarajiwa kuwepo inaweza isitosheleze mahitaji. Kutokana na hali hiyo, wizara itaendelea kufuatilia kwa karibu upatikanaji wa sukari nchini na kama upungufu utajitokeza, serikali itaruhusu uagizaji sukari kutoka nje nchi.
Kuhusu kilimo cha wakulima wadogo ambacho ni cha kujikimu, Waziri Chiza alisema ili kukibadilisha kilimo hicho kuwa cha kisasa na cha kibiashara ushiriki wa wakulima wakubwa na wa kati wenye mitaji, tekenolojia na ubunifu ni muhimu ili wakulima wadogo waweze kunufaika na ubia utakaotokana na ushirikiano huo.
“Hivyo ushiriki wa wakulima wakubwa na wakati hauna lengo la kuwafanya wakulima wakubwa kuwa mbadala wa wakulima wadogo. Lengo ni kujenga uhusiano kati ya wakulima wakubwa, wa kati na wadogo katika kutumia fursa zilizopo ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa mazao na upatikanaji wa masoko,” alisema Chiza.
Waziri huyo wa Kilimo, Chakula na Ushirika alisisitiza kuwa katika ubia huo wakulima wadogo hawatanyang’anywa mashamba yao ili kuwapa wakulima wakubwa.

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imeliomba bunge liidhinishe Shilingi 237,624,575, 000/=

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 21, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: