Advertisements
RSS

Tanzania kujifunza uzalishaji makaa ya mawe kwa Liberia‏

20 Jul

Arusha

NCHI ya Liberia na Tanzania zimekubaliana kuongeza ushirikiana katika masula ya kiuchumi na kijamii, ambapo kwa Tanzania imeonesha nia ya kujifunza  uzalishaji wa makaa ya mawe na zao la mpira kutoka nchi hiyo.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mahadhi Maalim, wakati alipokuwa akisoma taarifa fupi ya kumuaga Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kurejea nchini kwake, baada ya kuhitimisha ziara ya siku tatu nchini.

Rais wa Liberia, Ellen Johnson-Sirleaf akikagua gwaride la heshima la kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) PHOTO CREDIT: WAVUTI.COM BLOG

Alisema kuwa Liberia pia imeeleza hisia zake za kutaka kujifunza uzalishaji wa kahawa na mambo ya viwanda vya uvuvi nchini.

Mbali na masuala hayo, walizungumzia kuhusu amani na mshikamano katika nchi za Afrika, hasa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea Bissau, Mali na Somali, pamoja na kutafuta jinsi ya kutatua matatizo ya nchi hizo.

Aidha alisema Rais Ellen  akiwa ziarani nchini, Julai 18, aliitisha mkutano  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kuzungumzia kupambana na malaria na umuhimu wa wanawake katika kuendeleza Afrika.

Baada ya kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julai 19 alitembelea Arusha katika kiwanda cha A to Z kuangalia uzalishaji wa vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu, kwa lengo la kutokomeza malaria na pia alitembelea maabara ya utafiti wa magonjwa ya binadamu na mazao.

Hata hivyo baada ya ziara hiyo Rais huyo alimwalika Rais Jakaya Kikwete, kutembelea Liberia, ambapo Rais Kikwete aliupokea kwa furaha na kuahidi kuwasiliana kwa njia ya mtandao wao wa umma.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 20, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: