Advertisements
RSS

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Gregory teu Awataka Watanzania Kuchangamkia Fursa China

20 Jul

Beijing

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu amewataka Watanzania waache kulalamika, wachangamkie fursa za biashara zilizoko China.

Teu ametoa mwito huo leo (Ijumaa) kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Beijing, China, wakati anazungumza na wafanyabiashara, wakuu wa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na binafsi, waliokuwa wakishiriki Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Ushirikiano kati ya China na Tanzania  (FOCAC) uliomalizika jana.

Naibu Waziri amesema, China ni moja ya nchi zenye fursa nyingi za kufanya biashara na mataifa mbalimbali ikiwamo Tanzania, hivyo ni vyema kutumia fursa hiyo.

“Kwangu mimi, ningependa kuacha na mambo ya changamoto, changamoto, badala yake tutumie fursa. Tuache kulalamika, tuzamie huko,” amesema Teu.

Amesema, Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Watu wa China, Philip Marmo, amekaa Beijing kwa miezi miwili tu, lakini amefanya kazi nzuri sana.

“Lazima muitumie fursa hii ambayo Balozi ameijenga hapa, tuzitumie ili tukasaidie nyumbani, itatusaidia sana, tuwe wazalendo,” amesema Teu.

Amewataka watendaji hao na wafanyabiashara kutumia fursa hizo kwa manufaa ya vizazi vijavyo badala ya kuangalia wao wenyewe.

Mkutano huo nyumbani kwa Balozi Marmo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; na makatibu wakuu, Balozi Herbert Mtango (Ujenzi) na John Haule (Mambo ya Nje).

Waziri Membe pia alisisitiza suala la Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo China na kutafuta masoko ya bidhaa zao na pia kuwataka wasindike bidhaa zao, badala ya kuuza zikiwa ghafi.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 20, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: