Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Hakuna sera ya kuzuia kuuza mazao nje ya nchi‏

20 Jul

Dodoma

SERIKALI leo imelieleza Bunge kuwa haina sera ya kudumu ya kuwazuia wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira, ametoa msimamo huo wakati anajibu swali la Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (CCM).

Mhagama alitaka kufahamu ni lini serikali itajenga soko kubwa la kimataifa katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji ili kuuza mazao yao kwa bei nzuri.

Wasira amesema, serikali haioni ubaya kwa mpango wa kujenga soko la kimataifa la mazao katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili hatua ambayo alisema itawanufaisha wakulima.

Amesema, hata hivyo serikali inaowajibu wa kuhamasisha wakulima kuongeza juhudi katika uzalishaji wa chakula ili kuiwezesha nchi kuwa na ziada ya chakula hatua itakayowezesha wakulima kuruhusiwa kuuza chakula nje.

“Serikali haina sera ya kudumu ya kuwazuia wakulima kuuza chakula nje. Hatua hii huchukuliwa pale inapotokea kuwa nchi inakuwa na uhaba mkubwa wa chakula na hivyo kutishia uwezekano wa kuzuka kwa baa la njaa.

“Kama uzalishaji utaongezeka bila shaka tutakuwa na kiasi kikubwa sana cha chakula na hivyo tutaweza kuuza chakula hicho kwa nchi za jirani ambazo zinatutegemea sana katika kuwapatia chakula kutokana na Tanzania kuwa na eneo kubwa la ardhi linalofaa kwa kilimo,” alisema Wasira.

Alisema ili kuongeza uzalishaji, utoaji wa elimu bora ya kilimo cha kisasa, utumiaji wa mbegu bora za kisasa pamoja na utumiaji wa zana bora za kilimo cha kisasa ni baadhi tu ya maeneo yanayoongeza uzalishaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kuboresha hifadhi ya chakula.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 20, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: