Advertisements
RSS

Zanzibar: Waziri agoma kuwasilisha muswada wa sheria ya mafuta na gesi‏

18 Jul

Zanzibar

WAZIRI Mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Maji, Makazi, Nishati na Umeme, Ramadhan Abdalla Shaaban amewaeleza  wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa, hawezi kuwasilisha muswada wa sheria ya mafuta na gesi katika baraza hilo kwa kuwa Katiba hairuhusu.

 

Kiongozi huyo wa SMZ alikuwa anajibu hoja za wajumbe hao waliochangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Wawakilishi walimbana Waziri Shaaban na kumtaka awasilishe muswada wa sheria ambayo itaifanya Zanzibar kuruhusiwa kuanza kazi za kuchimba mafuta na gesi na kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali kufanya kazi hizo.

 

Waziri Shaaban amesema, ameapa kulinda Katiba mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo suala la mafuta na gesi limo katika orodha ya mambo ya Muungano.

“Mheshimiwa mimi nimekula kiapo kulinda Katiba mbili ile ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ambayo Katiba hairuhusu. Suala la mafuta na gesi limo katika orodha ya mambo ya Muungano hadi hapo Katiba itakaporekebishwa,” alisema Shaaban.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema bungeni mjini Dodoma kuwa, haoni tatizo kwa suala la mafuta na gesi kuondolewa katika masuala ya  muungano.

 

Shaaban ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wenye uzoefu wa muda mrefu katika chombo hicho, alisema suala la mafuta na gesi lipo katika hatua za mwisho za kupata ufumbuzi, hivyo aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa na subira ili kufahamu hatima ya suala hilo.

 

Akikariri kifungu cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 64(3) ambacho kinasema endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili.

 

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismali Jussa Ladhu (CUF), ndiye aliyeleta hoja hiyo wakati wajumbe walikaa kama Kamati kupitisha vifungu vya Bajeti ya Wizara ya Maji, Makazi, Ujenzi na Nishati, ambapo alisema yapo mambo ya orodha ya Muungano, lakini taasisi zake zimeanzishwa nchini. Aliyataja masuala ya bandari na anga.

 

Mapema, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa na subira wakati suala hilo likisubiri kupata baraka za mwisho kutoka Baraza la Mawaziri.

Advertisements
 
1 Comment

Posted by on July 18, 2012 in Business News, Tanzania News

 

Tags: , , , , , , , ,

One response to “Zanzibar: Waziri agoma kuwasilisha muswada wa sheria ya mafuta na gesi‏

  1. Pingback: Webmaster Guide

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: