Advertisements
RSS

Wakaguzi Wa Hesabu Watakiwa Kujinoa Zaidi

17 Jul

WAKAGUZI wa Hesabu za Serikali nchini wametakiwa kuwa wepesi wa kujifunza mbinu mpya mbalimbali za ukaguzi, ili watoe matokeo yanayoendana na mabadiliko ya kila siku katika mifumo ya matumizi ya fedha duniani.

Aidha, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) imesifiwa na kutajwa kuwa mfano wa kuigwa na nyingine za Afrika na duniani, kwa kuwa na ripoti za ukaguzi zenye viwango vya kimataifa.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh

Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali  za nchi 24 za Afrika zinazozungumza Kiingereza (AFROSAI-E), Wessel Pretorius, alisema  kutokana na mabadiliko duniani, wakaguzi hawana budi kubadilika ili kuwa chombo cha kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Kwa mujibu wa Pretorius, hilo litawezekana endapo wakaguzi watakuwa wepesi kujifunza na kubuni mbinu mpya za ukaguzi, kulingana na mabadiliko ya mazingira duniani, badala ya kukaa kusubiri wasukumwe na matokeo ya mabadiliko hayo.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Mpango wa Maendeleo ya Menejimenti (MDP) kwa mameneja wa NAOT, Pretorius alisema ili kupata matokeo mazuri ya ukaguzi pia ni lazima ofisi husika iwajengee watendaji wake wa chini busara ya kuwasikiliza mameneja na kushirikiana nao katika kazi.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hab Mkwizu alisema, Serikali inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inakuwa na uwezo wa kuendesha

shughuli zake wakati wote, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutosha.

Wakati akisema hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo aligusia mfumo wa bajeti unaotumika nchini na kusema kuwa unahitaji marekebisho ili uendane na wakati.

Kwa upande wake CAG, Ludovic Utouh alisema ofisi yake itaendelea kutoa kipaumbele cha mafunzo kwa watendaji wake ili kuwajengea

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 17, 2012 in Business News, Tanzania News

 

Tags: , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: