Advertisements
RSS

MIC yashinda mashindano ya biashara ya G20‏

17 Jul

Dar es Salaam

KAMPUNI ya Tigo imetangaza kuwa Shirika la Simu la Kimataifa (MIC), limetambulika kama moja ya washindi 15 katika mashindano ya G20 katika kipengele cha ubunifu wa biashara.

Changamoto hiyo ilizinduliwa kama moja ya mashindano na Rais wa Mexico wakati wa mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika Novemba 3 hadi 4, mwaka jana.

MIC ambayo ni Millicom International Cellular S.A, imekuwa ikitambulika kwa kutoa huduma za simu za mkononi kwa urahisi na kwa watu wa kipato cha chini katika nchi zinazoendelea kwa kuitangaza Tigo na huduma zake katika upatikanaji wake ndani ya masoko yake 13 yaliyojitokeza Afrika na Amerika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Guitierrez, uanzishwaji wa huduma za fedha za Tigo hivi karibuni imetambuliwa kama njia ya kuwezesha utumaji na upokeaji wa fedha kwa ajili ya wakazi wasio na huduma za kibenki.

“Ndani ya Tanzania pekee ambapo zaidi ya watu milioni 10 wanamiliki simu za mkononi, Tigo tayari iko katika nafasi nzuri ya kudumisha uongozi wa kanda yake katika sekta ya mawasiliano kutokana na huduma na bidhaa nyingi zenye viwango, zinazoendana na bidhaa zinazojulikana na zenye huduma ya kuridhisha kwa wateja wake.

‘’Ni furaha tele kwa kuweza kupata tuzo hii ya kifahari ambayo inatambua ubunifu wetu na mchango wetu kifedha, katika mazingira na jamii endelevu,” alisema Guitierrez.

Washindi wa kinyang’anyiro hicho walitangazwa na kupewa tuzo katika kilele cha Mkutano wa Viongozi wa G20 mjini Los Cabos, Mexico Juni 18, mwaka huu. Jopo la majaji la wataalamu 12 mashuhuri wa kimataifa kutoka katika sekta binafsi, wasomi, mashirika ya kimataifa na G20 walichagua washindi 15.

 

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 17, 2012 in Business News

 

Tags: , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: