Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Serikali yakataa kubadili uamuzi wa kuuza nyumba zake‏

14 Jul

Dodoma

BAADHI ya wabunge wameiomba Serikali ibadili uamuzi wake wa kuuza nyumba za watumishi na ikiwezekana izirejeshe nyumba za Serikali ilizoziuza ili Watanzania wengine nao wanufaike nazo badala ya wachache.

Hata hivyo, Serikali imebainisha wazi kuwa haina mpango wa kupitia uamuzi wake ili kurejesha nyumba zilizouzwa kwa watumishi wake kwa kuwa uamuzi wa kuuza nyumba hizo ulikuwa halali.

Katika swali la msingi Mbunge wa Mbulu Mustapha Akunay (Chadema), alisema kutokana na kitendo cha Serikali kuuza nyumba za Serikali za watumishi mwaka 2002-2005 kwa sasa watumishi wengi wanaohamishwa vituo nchini wanakosa nyumba za kuishi.

“Je Serikali ina mpango gani wa kupitia upya uamuzi huo na kurejesha nyumba zilizokuwa za Serikali?” Amehoji Akunai leo bungeni mjini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalumu Magdalena Sakaya (CUF), alisema nyumba hizo ziliuzwa kwa watumishi hao kwa bei ya kutupwa wakati zilikuwa katika maeneo maalumu hivyo ni muhimu zirejeshwe serikalini ili Watanzania wengine nao wanufaike nazo.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge, alisema uamuzi wa kuuza nyumba hizo ulifikiwa kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume ya ADAU ya mwaka 1963, Tume ya Nsekela mwaka 1975 na Tume ya Mramba ya mwaka 1984.

Alisema nyumba hizo ziliuzwa na Serikali kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupunguza gharama za kuhudumia nyumba zilizokuwa za siku nyingi, kuwawezesha watumishi hao walioitumikia Serikali kuishi katika nyumba bora na kuijengea uwezo Wakala wa Taifa wa Nyumba (TBA) kujenga nyumba zaidi.

“Utaratibu wa kuuza nyumba hizi ulifanyika baada ya uchambuzi wa kina uliojumuisha kuangalia uzoefu wa nchi nyingine, Bunge na tume zilizotoa ushauri wa kitaalamu kuhusu namna bora ya kupunguza tatizo la nyumba za Serikali,” alisema Lwenge.

Alikanusha nyumba hizo kuuzwa kwa bei ya kutupwa na kudai kuwa hiyo si hoja sahihi ambapo alisisitiza msimamo wa Serikali ni kutozirejesha  nyumba hizo na iwapo kuna mtu anapinga awasilishe hoja rasmi bungeni ili suala hilo lijadiliwe.

Aidha alisema majengo yaliyo chini ya TBA hadi sasa ni 2,713, kati ya nyumba hizo 1,353 zimepangishwa kibiashara, nyumba 748 zinapangishwa watumishi wa umma, nyumba 416 zinakaa viongozi, nyumba 103 ni za wageni, 56 ni majengo ya ofisi na nyumba 37 ni ikulu ndogo.

Related Links 

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 14, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: