Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Sheria Kuwabana Wafanyabiashara Wanaotumia Dola Nchini

12 Jul
Kutoka Bungeni: Sheria Kuwabana Wafanyabiashara Wanaotumia Dola Nchini

SERIKALI  inapanga kuipitia upya Sheria ya Fedha ili kuwabana wafanyabiashara nchini wanaotumia zaidi dola kuliko Shilingi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa , Serikali itafanya hivyo kukabiliana na kushuka kwa thamani ya Shilingi.

Waziri Mgimwa ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Bakari (CCM) aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kudhibiti matumizi holela ya dola nchini.

Katika swali lake Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya kushuka kwa Shilingi ya Tanzania ni matumizi makubwa ya dola kwa takribani kila kitu.

“Siku hizi kila kitu tunalipa kwa dola, uwanja wa ndege tiketi tunalipa kwa dola hata shuleni kwa dola, Serikali inadhibitije matumizi haya?

Akijibu swali hilo, Dk Mgimwa alisema kama Serikali katika kutatua tatizo hilo itazingatia zaidi kuangalia Sheria ya Fedha iliyopo inazungumza nini kuhusu matumizi makubwa ya dola nchini na iwapo ina upungufu katika hilo irekebishwe.

Alisema pia wataangalia sheria hiyo inazungumza nini kuhusu kumruhusu Mtanzania kuweka akiba ya dola badala ya Shilingi.

“Lakini pia kwa upande wa pili, Serikali tunayafahamu malalamiko mengi kuhusu matumizi ya dola na tumejipanga kuyashughulikia,” alisema.

Katika swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alitaka kujua Serikali inadhibitije biashara ya maduka ya kubadilisha fedha yasitumike kama mirija ya kusafirishia dola nje ya nchi kinyume cha sheria.

Lakini pia mbunge huyo aliitaka Serikali ibainishe mikakati yake itakayokwamua wafanyabiashara wa ndani na kudhibiti ununuzi wa bidhaa zinatengenezwa nchini, kununuliwa kutoka nje huku akitolea mfano vijiti vya kuchokonoa meno.

Akijibu swali hilo, Dk Mgimwa alisema zipo sheria na taratibu zinazotumika kuongoza maduka hayo namna ya kufanya kazi na hadi sasa vyombo vinavyotumika kudhibiti maduka hayo havijatoa taarifa yoyote ya kuonesha kuwa maduka hayo yamekuwa yakifanya biashara zake kinyume na taratibu zilizopo.

“Lakini bado hoja inabaki palepale kuwa maduka haya yanatuhumiwa kufanya kazi kinyume na taratibu, Serikali tanayachukua malalamiko yote na kuyafuatilia lengo likiwa ni kuhakikisha yanafanyakazi inavyotakiwa,” alisisitiza.

Soma Hapa Taarifa Zaidi ya Bajeti ya Tanzania

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 12, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: