Advertisements
RSS

Wajasiliamali Acheni kulalamika – Mapunjo

09 Jul

Arusha

WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kubuni mbinu mbalimbali za biashara zitakazowezesha kupata masoko badala ya kulalamikia bidhaa kutonunuliwa.

Aidha wametakiwa kutumia alama ya kutambulisha bidhaa walizozalisha kutokana na alama hiyo kuhifadhi kumbukumbu ya mahali inapotoka bidhaa, mzalishaji na mtumiaji wa bidhaa hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko,Joyce Mapunjo alisema hayo karibuni wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku nne kwa wajasiriamali kutoka Kenya, Tanzania na Nigeria kwa ajili ya kutambulisha alama mpya itakayomtambulisha mjasiriamali aliyetengeneza bidhaa mbalimbali.

Mapunjo alisema Serikali inajitahidi kuwainua wajasiriamali ili wapate masoko lakini cha kushangaza badala ya kubuni mbinu zitakazowawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora, huishia kuiga biashara na kulalamikia masoko.

Alisema ni vyema wajasiriamali waachane na tabia hiyo badala yake wawe wabunifu, ili wapate soko na kushindana na masoko ya ndani na nje ya nchi hususan Kenya, kwani wao wamefanikiwa kuuza bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi kutokana na kutumia alama maalumu kwenye bidhaa zao.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya GSI (TZ), Elibariki Mmari alisema alama hiyo itawezesha Tanzania kujulikana duniani kuwa miongoni mwa nchi zinazozalisha bidhaa mbalimbali.

Advertisements
 
2 Comments

Posted by on July 9, 2012 in Tanzania News

 

Tags: ,

2 responses to “Wajasiliamali Acheni kulalamika – Mapunjo

 1. Happy Joseph

  July 22, 2012 at 12:47 am

  title ya hii article haijakaa vema..kwa uelewa wangu mdogo wa kiswahili ni ‘wajasiriamali’ instead of ‘wajasiliamali’

   
  • monfinance

   July 23, 2012 at 1:45 pm

   Nashukuru kwa Mawazo Happy, Nitalifanyia kazi na Kurekebisha. Karibu tena na endelea kutupa comments na kutembelea MonFinance.

    

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: