Advertisements
RSS

CTI Yazindua Mradi wa utafiti wa Biashara

09 Jul

SHIRIKISHO la Wenye Viwanda (CTI) limeelezea haja ya kuendelea  kutengeneza mazingira bora ya biashara ili kufanya bidhaa zinazozalishwa nchini zikiwemo za huduma kushindana kimataifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Christine  Kilindu ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya hali halisi ya mazingira ya  kibiashara nchini.
Taarifa hiyo ni matokeo ya utafiti uliofanywa  kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini kwa mwaka jana .Taarifa hiyo ni ya nne tangu CTI kwa kushirikiana na BEST-AC katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya biashara nchini.
Katika taarifa hiyo mambo manne  yalielezwa kukwamisha hali bora ya uwekezaji nchini. Mambo hayo ni  tatizo la nishati ya kuaminika, uhafifu wa barabara, rushwa, upatikanaji wa maji usiokuwa na uhakika, fedha na kodi zinazopandiana.
Alisema utatuzi wa vikwazo vya biashara nchini kutasaidia wawekezaji wote wa  ndani na watokao nje ya nchi kutengeneza bidhaa zenye ushindani na  kuwezesha mabadiliko makubwa yanayohitajika katika uchumi wa Tanzania.
“ Kumekuwepo na mabadiliko madogo kama yanavyoonekana kwenye Ripoti ya  Biashara ya Benki ya Dunia ambapo kwa mara kadhaa Tanzania imekuwa  ikishika nafasi ya chini. Ripoti hizi zinaonesha kuwa, Tanzania ni  mahali pagumu sana katika kuwekeza na kufanya biashara.”
Alisema  na kuongeza kuwa mitazamo ya viongozi wa biashara ambayo imetolewa kwa  lengo mahsusi la kuchukua maoni ya jumuiya za biashara za Tanzania pia  imeainisha ugumu uliopo wa kufanya biashara nchini.
Christine  alisema ni matumaini yake kwamba changamoto zilizoelezwa katika ripoti  hiyo zitafanyiwa kazi na kuisogeza Tanzania katika mazingira bora zaidi  za ufanyaji biashara na uwekezaji.
Katika hafla hiyo wachora vibonzo walipewa tuzo zao zikiwemo fedha taslimu kwa jinsi  walivyoweza kusaidia katika ushawishi wa mabadiliko kwenye sera na  kanuni za uendeshaji biashara nchini

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 9, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: