Advertisements
RSS

Vodacom yatumia Zaidi ya mil.120 kuboresha mawasiliano‏ Maonyesho ya Sabasaba 2012

05 Jul

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imesema imetumia zaidi ya Sh  milioni 120 kuboresha sekta ya mawasiliano katika Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kelvin Twisa – Mkuu wa masoko na mawasiliano wa Vodacom


Imesema fedha hizo zinatumika katika kuwezesha mawasiliano na machapisho  mbalimbali katika maonesho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Tuzo ya udhamini wa  maonyesho hayo, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin  Twissa, alisema kuwa fedha hizo zinatumika katika kuzalisha machapisho na  mawasiliano kwa vyombo vya habari katika maonesho hayo.

“Tunatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kutangaza Maonesho haya ya  Kimataifa ya Sabasaba kwani yanakusanya watu wengi kutoka sehemu mbalimbali na  vyombo vya habari vinao mchango mkubwa katika kutoa taarifa kwa Watanzania ndio  maana tumeamua kuwekeza kiasi hiki cha pesa katika kuhakikisha masuala yote ya  mawasiliano yanafanyika vizuri ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa katika  maonyesho haya,” alisema Kelvin .

Maonesho ya Sabasaba yanayodumu kwa siku 10, hukusanya watazamaji zaidi ya  350,000 na kutoa fursa kwa watazamaji kulinganisha ubora wa bidhaa na kufanya  ununuzi.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 5, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: