Advertisements
RSS

Ecobank Kuendelea Kuikopesha NHC Ijenge Nyumba

05 Jul

BENKI ya Ecobank imeahidi kuendelea kulikopesha zaidi Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), katika mradi wa kujenga nyumba na kukopesha ili kuhakikisha Watanzania  wengi wanapata nyumba bora na za bei nafuu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.


Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, James  Cantamantu-Koomson, ametoa ahadi hiyo wakati baada ya hafla  iliyoandaliwa na NHC kwa ajili ya kutiliana saini mkataba wa mkopo na taasisi  tisa za fedha juzi jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, Ecobank ilisaini kutoa mkopo wa Sh bilioni 2.1 na imeahidi  kuwa itaongeza kiasi kingine cha fedha siku zijazo ili kufanikisha mradi huo  wenye manufaa kwa wananchi.

Mkurugenzi huyo alisema Ecobank inawajali Watanzania na imeahidi kuunga mkono  kwa dhati mpango huo wa NHC ili kuwakomboa Watanzania wengi ambao hawana makazi  bora kutokana na kipato kidogo.

“Sisi Ecobank mradi kama huu si mgeni kwetu, tunajali na kuthamini sana  masuala ya makazi, karibu nchi zote 30 tunazofanya kazi zetu tunashiriki miradi  kama hii, kuwapa wananchi nyumba bora ni jambo la muhimu sana,” alisema.

Ndugu Cantamantu-Koomson alisema ingawa benki hiyo ina miaka miwili tu tangu ianze kutoa huduma zake  nchini, imejitahidi kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya Watanzania na kushiriki  katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Mwishoni mwa mwaka 2011, NHC ilipewa kibali na Serikali kukopa kwenye taasisi  za fedha za ndani na nje ya nchi ili kuendeleza miradi ya ujenzi

Kwa ujumla Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limesaini mikataba ya mkopo wa Sh bilioni 165 kutoka kwa taasisi nyinginezo  tisa za fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa miradi ya ujenzi wa nyumba pamoja na ununuzi wa ardhi ya akiba.

Taasisi za fedha zilizotoa  mkopo huo pamoja na kiwango walichotoa kwenye mabano ni pamoja na CRDB (Sh bilioni 35), ECO Bank (Sh bilioni 2.1), TIB (Sh bilioni 22), BancABC  (Sh bilioni 4.2), NMB (Sh bilioni 26), CBA (Sh bilioni 24), LAPF (Sh bilioni  15), Azania (Sh bilioni saba) na Shelter Afrique (Sh bilioni 23).

Advertisements
 
1 Comment

Posted by on July 5, 2012 in Business News, Tanzania News

 

Tags: , , , , , , , , , , , , ,

One response to “Ecobank Kuendelea Kuikopesha NHC Ijenge Nyumba

 1. Derrick

  July 5, 2012 at 4:07 pm

  Shirika la Nyumba la Taifa si sawa na benki binafsi eg. CBA. For one thing, NHC ni shirika la umma. Lengo lake si kuingizia serikali mapato. Bali ni kutoa huduma kwa watanzania. Yes. Linapaswa kujiendesha kwa faida lakini lengo kuu si profit maximization. Unapoendesha shirika hili, ambalo waasisi wake walilenga watu wenye kipato cha kawaida, kama benki ya biashara unakuwa unaongozwa na malengo ya kutengeneza faida kubwa ili usifiwe na kuwasahau walengwa ambao ni Watanzania wa kipato cha kawaida. Huyu Bwana amelichukua Shirika likiwa halina uwezo wa kifedha (so they say). Hivyo, akaamua kuja na style ya kujenga nyumba kwenye “prime plots” za shirika hili na kuziuza ili kujenga uwezo wa kifedha (ninaambiwa hata mtumishi wa NHC ni shughuli kupata nafasi ya kuuziwa nyumba hizo, if you know what I mean). Fine. Uwezo wa kifedha utaongezeka (if it works) lakini asset za shirika zitapungua. Kupungua kwa assets za shirika kunapelekea kufa kwa shirika, regardless of how much money you have at hand. Na kumbuka kutengeneza faida kubwa si lengo la shirika.

  Lengo la shirika ni kuwapatia Watanzania makazi bora kwa gharama nafuu. Kabla ya huyu bosi kuongoza Shirika na inavyofanyika nchi nyingine, Shirika hili linapaswa kujenga makazi bora ya gharama nafuu na kuendesha renting business. Watanzania walio wengi watamudu kulipa gharama ya pango kila mwezi lakini hawawezi kumudu kulipa Shilingi 100 million kwa mkupuo. Hawakopesheki. Hii itaondoa matatizo mengi sana. Itapunguza rushwa. Itaongeza ufanisi wa kazi. Badala ya mfanyakazi kufikiria namna ya kuiba ili aweze kujenga nyumba au kununua nyumba ya NHC, atatulia na kufanya kazi. Kwa sababu uhakika wa makazi anao. Na usipolipa pango kwa mwezi, unatolewa anapewa mtu mwingine. This is how it should work. NHC isishindane na mabenki kutengeneza faida kubwa. Hili ni shirika la umma. Lilenge kutoa huduma zaidi. And yes. Linastahili ruzuku ya serikali at some point (economists hate subsidy arguing it’s an inefficient way to allocate resources. But who doesn’t do it?).

  Na NHC ikifanya kazi yake vizuri, gharama ya pango inayotozwa sokoni kwa sasa itaji-regulate vizuri sana. Kwa sasa wenye nyumba wanatoza bei yeyote wanayotaka. Hakuna wa kumuuliza. Na kwa kuwa kuna shida ya makazi, watu wanaishia kuiba ili kumudu gharama za pango. Mishahara haiendani na gharama za pango sokoni. Watu wanamudu vipi kulipa kama si kwa kuiba?

  Bw. Mchechu, NHC ni mkombozi wa Watanzania linapokuja swala la makazi.Jitahidi kuhudumia Watanzania wenye mahitaji na si matajiri wanaotafuta kujilimbikizia mali. Kwa kuuza maeneo mazuri ya NHC, huna tofauti na wale waliojiuzia nyumba za Serikali. We are counting on you!

   

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: