Advertisements
RSS

Twiga Bancorp kufanya kazi Masaa 24

02 Jul

UONGOZI wa Benki ya Twiga Bancorp umesema tawi lake la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini litaendelea kutoa huduma kwa saa 24 kila siku ili kukidhi mahitaji ya wateja.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga Bancorp, Hussein Mbululo amesema hayo hivi karibuni wakati akizungumzia tuzo ambayo benki hiyo ilipokea kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Business Initiative Directions ya Geneva, Uswisi.

Alisema benki hiyo yenye matawi Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma, inaendelea kujitanua kwa kufungua tawi moja mkoani kila mwaka.

Alisema hivi karibuni itafungua tawi mkoani Dodoma. “Tawi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, linaendelea kuvunja rekodi ya kufunguliwa kwa saa 24 kwa siku zote saba za wiki,” alisema Mbululo.

Alisema mtandao wa huduma kwa benki hiyo umeimarika kutokana na kadi zake za ATM kuunganishwa na mtandao wa Umoja unaoziunganisha benki zaidi ya 24, zikiwa na mtandao wa zaidi ya mashine 160 nchini. A

kizungumzia tuzo ya Century International Gold Quality waliyoipata, alisema huduma ya ‘Money gram’ wanayotoa ndiyo imewezesha kuipata.

Alisema huduma hiyo inawawezesha Watanzania na watu wa mataifa mengine kutuma fedha nje kwa dakika chache. “Walieleza kuridhishwa na huduma zetu kufikia kiwango cha ubora wa juu lakini pia walieleza kuridhishwa na ubunifu tunaoendelea kuufanya katika kuboresha huduma za kibenki nchini ukilinganisha na benki nyingine,” alisema Mbululo.

Kwa mujibu wa Mbululo, kupitia huduma za Money gram mtu anaweza kutuma fedha kwa mtu aliye nje ya nchi na kuzipata ndani ya dakika tano.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 2, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: