Advertisements
RSS

Wanahisa Waiagiza CRDB ifungue Matawi Nje ya Nchi

26 Jun

WANAHISA takriban 10,000 wa benki ya CRDB wameuagiza uongozi wa benki hiyo kupanua wigo wake wa kufungua matawi nje ya nchi hususani katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati ili mtaji upanuke.


Walitoa mwito huo katika mkutano mkuu wa 17 wa wanahisa uliofanyika mjini Arusha na kusema kwa kufanya hivyo kutaifanya benki hiyo kutambulika zaidi kimataifa na kuaminika.

Mkurugenzi wa CRDB Dk Richard Kimei alisema suala hilo wamelichukua kama changamoto kwao na kwa kuanzia wameshafanya utaratibu wa kufungua tawi la benki hiyo nchini Burundi. Kimei alisema kufungua benki katika nchi hiyo haitakuwa tatizo kwa kuwa wana mtaji wa zaidi ya Sh bilioni 254.

Alisema mtaji umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kwa zaidi ya miaka minne na kuifanya ikubalike ndani na nje ya nchi.

Alisisitiza kwamba maoni ya wanahisa ya kutaka yafunguliwe matawi katika nchi za ukanda, hayatashindikana. Alisema licha ya mtaji kuongezeka, pia rasilimali za benki zimekuwa zikiongezeka kwa asilimia 20 tofauti na miaka iliyopita.

Alisema benki ya CRDB ina rasilimali yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni 2,713.6 na rasilimali hizo zimekuwa zikiongezeka mwaka hadi mwaka.

 Wakati huo huo alisema benki hiyo imepata faida ya zaidi ya Sh bilioni 37.8 na gawiwo kwa wanahisa ni zaidi ya Sh bilioni 19.6. Alisema mwaka jana uwekezaji wa benki kwenye dhamana za Serikali uliongezeka kwa Sh bilioni 117 ikilinganishwa na Sh bilioni 86 kwa mwaka juzi.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 26, 2012 in Uncategorized

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: