Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Gesi Kuwakomboa Watanzania – Simbachawene

26 Jun

NISHATI ya gesi ina nafasi kubwa kuibadili Tanzania kwa haraka endapo itatumika ipasavyo, Bunge limeelezwa.

Huge Gas Discoveries Offshore Tanzania

Huge Gas Discoveries Offshore Tanzania

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amewaeleza wabunge kuwa, watanzania wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwajalia gesi kwa kuwa itabadili maisha ya watu, itawezesha kupatikana mbolea, kuongeza kasi ya utekelezaji wa sera ya kilimo Kwanza, na kuiwezesha nchi kupata umeme wa kutosha.

Simbachawene ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Viti Maalum, Amina Nassoro Makilagi, ni lini gesi itawanufaisha Watanzania hasa wanawake na vijana, na Serikali ina mikakati gani kuhakikisha makundi hayo yanashiriki kuchimba nishati hiyo badala ya kuwa watazamaji tu.

Awali wakati anajibu maswali ya msingi ya Mbunge huyo, Simbachawene alisema, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ipo katika hatua za mwisho za kuandaa sera, sheria na mpango kabambe wa matumizi ya gesi.

“Wizara inashirikiana na Mshauri Mwelekezi taasi ya Research on Poverty Alleviation (REPOA) kwa ajili ya kupitia rasimu ya Sera ya Gei asili. Mshauri mwelekezi huyo ameanza kazi tangu mwezi Mei, 2012 na anatarajia kukamilisha kazi hiyo mwezi Septemba, 2012” amesema Simbachawene.

Kwa mujibu wa Simachawene, kwa kuwa rasimu ya sheria ya gesi iliandaliwa hata kabla ya kuwepo kwa Sera ya Gesi, Wizara inakusudia kuiangalia upya rasimu hiyo ili kujiridhisha kuwa haikinzani na Sera mpya ya gesi asili.

“Hiyo inategemewa kuwa Muswada wa Sheria ya Gesi asili utakuwa tayari kuwasilishwa bungeni mwezi mmoja baada ya Sera ya Gesi Asili kukamilika”amesema.

Simbachawene amesema, watalaamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwa kushirikiana na Mshauri mwelekezi kutoka Trinidad and Tobago, wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha rasimu ya mpango kabambe wa matumizi ya gesi na kwamba, unatarajiwa kukamilika sambamba na Sera ya Gesi asili.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amelieleza Bunge kuwa, kasi ya utafutaji na ugunduzi wa gesi asilia imeongezeka na kwamba, hivi karibuni kampuni zinazofanya utafiti wa gesi asilia nchini zimegundua kiasi kikubwa cha nishati hiyo chenye ujazo wa trilioni 3.

“Gesi hiyo imegundulika kwenye kina cha maji marefu baharini takriban kilomita 80 kutoka nchi kavu mashariki mwa mkoa wa Lindi. Ugunduzi huo unafanya kiasi cha gesi kilichogundulika hadi sasa kwenye kina cha maji marefu baharini  kufikia futi za ujazo trilioni 20.97” amesema Pinda wakati anawasilisha bungeni mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Pinda amesema, Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba taifa linanufaika kikamilifu na ugunduzi wa rasilimali hiyo, na kwamba, itawawezesha vijana nchini kupata mafunzo maalum yanayohusiana na masuala ya gesi asilia ili Tanzania iwe na wataalam wazalendo waliobobea katika sekta hiyo kama ilivyoainishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 26, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: