Advertisements
RSS

Tanzania: Thamani Ya Bidhaa za Kilimo Yaongezeka

24 Jun

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu amesema, thamani hiyo imeongezeka kutoka Sh bilioni 410 mwaka 2007 hadi Sh trilioni 1.07 mwaka 2011.
 
“Kwa mujibu wa taarifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Mamlaka ya Mapato kwa kipindi cha mwaka 2007/2011, bidhaa za kilimo zilizouzwa nje ni pamoja na kahawa, pamba, katani, chai, tumbaku, korosho na karafuu,” amewaeleza wabunge mjini Dodoma.
 
Alikiri kuwa thamani ya Shilingi itapanda endapo uuzaji wa bidhaa nje utaongezeka, na hii itategemea kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa kiasi kikubwa kukidhi soko la ndani na baadaye ziada kuuzwa nje.
 
Alisema Serikali imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wawekezaji wa ndani na nje kuuza bidhaa zao nje kupitia Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji (EPZA) kwa kutenga na kuendelea kuwatengea wawekezaji maeneo ya uzalishaji katika mikoa yote nchini.
 
“Aidha, tangu kuanzishwa kwa Mpango wa EPZ mwaka 2002 hadi hivi sasa (2012), makampuni 40 kati ya makampuni 54 ya ndani na nje ya nchi yamekuwa yakizalisha kwa utaratibu uliowekwa na Mamlaka ya EPZA,” alisema.
 
Aliitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na maonesho ya Sabasaba, Nanenane na maonesho ya kikanda yanayosimamiwa na kuratibiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ambayo hufanyika kila mwaka.
 
Naibu Waziri alisema, lengo la maonesho hayo ni kuwapa fursa wafanyabiashara kutangaza na kupata masoko ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
 
Wakati huohuo, Rwanda na China zimetajwa kuwa nchi zitakazoshiriki kwa kiwango kikubwa katika maonesho ya biashara ya Sabasaba yanayotarajiwa kuanza kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (TanTrade), Samwel Mvingira ameyasema hayo wakati akizungumzia ubia kati ya taasisi yake na Kampuni ya simu ya Vodacom katika mawasiliano.
 
Mvingira alisema nchi hizo zimejitokeza zaidi katika ushiriki ikilinganishwa na nchi nyingine za kigeni.
 
Alisema wafanyabiashara kutoka Rwanda wamechukua meta za mraba 400 zinazoweza kutumika kwa watu zaidi ya 45 wakati China imechukua takribani meta za mraba 1,000.
 
“ Imekuwa tofauti na maonesho ya mwaka jana, kwa Rwanda inaonesha wamehamasishwa sana kuja kuonesha na kufanya biashara na kwa upande wa China wamekuja kushiriki na wataendesha pia maonesho yao ndani wakati haya yetu yakiwa yanaendelea,” alisema na kuongeza kuwa maonesho ya China yataanza Julai 1 hadi 5.
 
Mvingira alisema, nchi 11 zimejitokeza kushiriki maonesho hayo huku kampuni za ndani zikiwa 1,500, za nje 435 na taasisi za serikali zipatazo 64.
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom, Joselin Kamuhanda alisema kampuni yake inatarajia kutumia zaidi ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kuendesha matangazo ya maonesho kwa siku 10.

Posted by MJ

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 24, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , , , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: