Advertisements
RSS

Kutoka Bungeni: Serikali Kulinda Viwanda Vya Ndani

24 Jun

Serikali imekubali mapendekezo ya wabunge ya kuongeza kima cha chini cha mapato ya wafanyabiashara yanayotozwa kodi kutoka shilingi milioni tatu hadi milioni nne.
 
 Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amesema, uamuzi huo wa Serikali utawawezesha wafanyabiasha wadogo wakiwemo waendesha ‘bodaboda’ kujiendeleza kibiashara.
 
Amewaeleza wabunge mjini Dodoma kuwa, Serikali pia imekubali ushauri wao wa kuongeza kodi ya mafuta ya kula kwa mafuta yanayoagizwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani.
 
Kwa mujibu wa Waziri Mgimwa, uamuzi huo wa Serikali sasa utawasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
 
“Lakini Serikali imekubali mapendekezo ya waheshimiwa wabunge” amesema. Kwa mujibu wa Waziri Mgimwa, Serikali kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa viwanda vinavyozalisha nguo kwa kutumia pamba inayolimwa nchini.
 
“Tumeikubali hiyo hoja, tunaifanyia kazi” amelieleza Bunge na kubainisha kwamba, uamuzi huo utasaidia kuongeza ajira nchini na mapato ya wananchi.
 
Amesema, Serikali inafanya uchambuzi wa suala hilo ili kuona ni wapi itafidia , na kwamba, itatoa ufafanuzi wa jambo hilo katika Muswada wa Fedha wakati wa Mkutano unaoendelea wa Bunge mjini Dodoma.
 
Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira amewataka wanunuzi wa pamba kutowatwisha mzigo wa kila kitu wakulima wa pamba wakati bei inaposhuka katika soko.
Amesisitiza kwamba, suala la kufufua viwanda ni la msingi na Serikali itahakikisha viwanda vya nguo vinapewa kipaumbele na kuhakikisha malighafi zinazopatikana, zinatumika hapa nchini.

Wasira ameyasema hayo wakati akifanya majumuisho ya hotuba yake ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011/12 pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

“Nisingeweza kumaliza hotuba yake bila kuzungumzia pamba, wakulima wa pamba wasingenielewa, wao ndio wanaoniweka mjini,” alisema. “Wanunuzi wa pamba wasiwatwishe wakulima mzigo wa kila kitu wakati bei inaposhuka.

Ingekuwa busara kama wanapata faida ya asilimia kumi, basi wachukue asilimia 9 au 8 na inayobaki iende kwa mkulima.

Katika michango yao, wabunge waliitaka Serikali kuhakikisha bei ya pamba inaongezeka kutoka ya sasa ya kilo kwa Sh 520 kufikia Sh 1,000.

Akizungumzia hoja za wabunge kuhusu kufufua viwanda na kuviendeleza vilivyopo, Wasira alisema hicho ni moja ya kipaumbele cha Bajeti ya 2012/13, hivyo Serikali itahakikisha inavilinda viwanda vya nchini.

“Msimamo wa Serikali uko wazi, viwanda ni mojawapo ya vipaumbele vilivyoainishwa katika bajeti hii. Kwa hiyo, tutahakikisha viwanda vyetu vinafufuliwa na vinavyofanya kazi vinaendelezwa,” alisema Wasira.

Posted by MJ

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 24, 2012 in Uncategorized

 

Tags: , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: