Advertisements
RSS

Tanzania: Gesi Yagundulika Lindi

19 Jun

Dodoma, Tanzania

WAKATI Serikali ikithibitisha kugundulika gesi yenye futi trilioni tatu za ujazo Mashariki mwa Lindi, imesema katika miaka mitatu ijayo, itatumia gesi kuzalisha umeme, kutumika majumbani na kuuzwa nje ya nchi.

“Kwa kweli tuna gesi ya kutosha sana … mipango ya Serikali ni kwamba katika miaka mitatu ijayo, tutazalisha gesi kwa ajili ya umeme, majumbani na viwanda vya mbolea,” alisema Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma kuhusu ugunduzi wa gesi asilia nchini wiki hii.

“Napenda sasa kuutangazia umma kuwa Juni 13, 2012, Kampuni ya Statoil ya Norway kwa kushirikiana na ya Exxon Mobil ya Marekani, ziligundua na kuthibitisha kuwapo kwa gesi yenye ujazo wa futi za ujazo trilioni tatu katika kisima cha Lavani kitalu namba mbili Mashariki mwa Lindi,” alisema Profesa Muhongo.

Amesema, hadi sasa gesi asilia iliyogundulika kwenye maji ya kina kirefu ni futi trilioni 20.97 za ujazo, huku Tanzania ikiwa imejaaliwa kuwa na gesi ya kutosha.
Imesisitiza kuendelea kutoa msukumo zaidi kwa ajili ya kampuni za utafutaji mafuta na gesi asilia ili ziendelee kufanya utafiti na ugunduzi zaidi wa gesi asilia na mafuta kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

“Aidha, kisima kilichochimbwa Songo Songo Kisiwani na kukamilika Mei 2012 kimebainika kuwa na uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 60 kwa siku. Hii ni hazina mpya nchini,” aliongeza Waziri wa Nishati na Madini na kusema kuwa, gharama za kisima kimoja ni kati ya dola milioni 100 na 150 za Marekani (kati ya Sh bilioni 160 na Sh bilioni 240).

Alisema katika miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji mafuta na gesi nchini, ambao umejikita zaidi kwenye bahari ya Hindi kwenye maji ya kina kirefu.

Alisema kuna kampuni kubwa duniani za utafutaji mafuta na gesi asilia nchini na hadi Juni 14, zipo kampuni 19 mbali na Antrim ambayo ina leseni Zanzibar ambako shughuli za utafiti hazifanyiki.

Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Petrobas ya Brazil, British Gas, Aminex, Ophir, Dominion, Wentworth Resources, Afren Rescources Petrodel (Uingereza), Exxon Mobil na Shell (Uholanzi), Statoil (Norway) na Maurel & Prom (Ufaransa).

Nyingine ni Heritage (Ireland), Jacka Rescources, Otto Energy, Swala Oil & Gas, Beach Petroleum (Australia), Motherland (India) na Hydrotanz (Mauritius).
Profesa Muhongo alisema kampuni hizo zinafanya kazi kwa upekee au kuungana na nyingine kwenye sehemu mbalimbali za leseni na utafiti na ambao unakwenda kasi kubwa ni wa kwenye bahari ya kina kirefu.

Alisema hivi sasa kuna mitambo mitano ya kuchimba visima vya utafiti wa mafuta na gesi, ambapo miwili inafanya kazi kwenye bahari ya kina kirefu na mitatu nchi kavu.
“Utafiti wa nchi kavu nao unaendelea vizuri ukijumuisha mitambo mitatu ambayo iko  nchini ikichimba visima. Vitatu vimekamilika. Viwili vikiwa vimegundua gesi Songo Songo na Magharibi mwa Mtwara.

“Kisima kimoja kilichochimbwa Mnazi Bay hakikuwa na gesi ya kutosha. Kisima kilichokamilika Mei 2012 Songo Songo kina uwezo wa kuzalisha meta za ujazo milioni 60,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema Wizara ya Nishati na Madini iko katika hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya Sera, Sheria na Mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia nchini.

Posted by MJ

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 19, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: