Advertisements
RSS

Bajeti ya Tanzania: Asilimia 80 ya mapato ya ndani yakusanywa kufikia April 2012.

18 Jun

MAKUSANYO ya mapato ya ndani yamefikia Sh bilioni 5,684.5 kufikia Aprili mwaka huu ikiwa ni sawa na asilimia 80 ya makadirio ya mwaka 2011/12.

Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa ameliambia Bunge wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/13.

Kwa mujibu wa Dk Mgimwa, makadirio yalikuwa ni kukusanya Sh bilioni 7,126.4 kwa mwaka wa fedha 2011/12 ambao unafikia kikomo Juni 30, 2012.

Aidha, alisema makusanyo ya kodi yalifikia Sh bilioni 5,227.5 ambayo ni sawa na asilimia 84 ya makadirio ya kukusanya Sh bilioni 6,228.8.

“Kulingana na mwenendo wa makusanyo ya mapato ya kodi kwa kipindi cha miezi kumi ya mwaka 2011/12, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha 2011/12, Serikali inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 6,307.8 na hivyo kuweza kufikia lengo tuliojiwekea,” alisema Dk Mgimwa.

Kuhusu mapato yasiyotokana na kodi, Waziri wa Fedha alisema yamefikia Sh bilioni 451.6 ikiwa ni sawa na asilimia 83 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 547.1 kwa mwaka.

Akizungumzia mapato ya Serikali za Mitaa, alisema yalifikia kiasi cha Sh bilioni 143 sawa na asilimia 40.8 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 350.5 kwa mwaka.

“Hadi Juni 2012, Serikali inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 200 kutokana na chanzo hiki ikiwa ni asilimia 57 ya lengo la mwaka,” alisema.

MF: Tutaendelea kupost vipande vipande vya Bajeti ya mwaka 2012/13 mpaka mwisho wa kikao cha bunge cha bajeti. Hii itasaidia kuilewa bajeti hiyo katika kila kipengele.   

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 18, 2012 in Business News, Tanzania News

 

Tags: , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: